DC KALAMBO AGIZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO KUWAWEZESHA WATOA HUDUMA  ZA AFYA NGAZI YA JAMII  KIUCHUMI









Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Lazaro Komba ameyasema hayo Tarehe 09.02.2023 wakati akifunga kikao kazi Cha kutathimini  Hali ya lishe katika Wilaya  Kalambo ambapo pamoja na Mambo mengine Suala la watoa huduma ngazi ya jamii kusuasua kukusanya takwimu za Maauala ya lishe   kutokana na changamoto ya Maslahi ikaibuka.  

Kimsingi watoahuma wahawa wanapaswa kufanya kazi kwa kujitolea lakini wakati mwingine wanalazimika kufanya kazi zao ili waweze kujikimu kimaisha hivyo hali hii inakwamisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu sahihi  jambo lililopelekea  mkuu wa Wilaya ya Kalambo kamwagiza mkurungezi wa Halmashauri  kuwawezesha kiuchumi ili wakufanye takwimu sahihi.